Pages

September 21, 2011

Baada ya kushutumiwa na Pinda, polisi waibuka na kujichimbia mkwara,


IGP Saidi Mwema akiwa na DCI Robert Manumba. 

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Robert Manumba amesema kuwa jeshi la polisi litawachukulia hatua kali askari wote wanaojiususha na magendo ya sukari, hii ni baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwashutumu hadharani kuwa kuna polisi wanahusika katika sakata zima la utoroshwaji wa sukari nje ya nchi na hivyo kusababisha uhaba usio na lazima. 


JWTZ Kuridhi polisi sakata la sukari 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewatuhumu polisi, kwamba wanahusika na utoroshaji wa sukari nje ya nchi na kulitaka Jeshi hilo kukomesha vitendo hivyo mara moja, vinginevyo Serikali italiagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuingilia kati ili kudhibiti vitendo hivyo.

 Akiwahutubia mamia ya wakazi wa hapa akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mara, Waziri Mkuu alisema Serikali haiwezi kulikalia kimya suala hilo huku wananchi wakiteseka.
 Alisema viwanda vya sukari vya Mtibwa na Kilombero vilivyopo mkoani Morogoro, Kagera na TPC cha Moshi, vinafanya kazi nzuri ya kuzalisha wastani mzuri wa sukari ambayoinatosha kwa matumizi ya wananchi, lakini sukari hiyo haipatikani nchini.

 “Viwanda hivi vinazalisha tani 41,000 hadi 44,000 wakati matumizi yetu ni wastani wa tani 30,000 na 31,000; hii inaonesha kwamba kuna karibu tani zaidi ya 10,000 za ziada. Lakini jambo la ajabu sukari haipatikani nchini na kuifanya kupanda bei na kuumiza wananchi,” alisema Pinda.

 Alisema amepewa taarifa za siri, kwamba baadhi ya polisi wanashiriki katika utoroshaji huo wa sukari kwenda nchi jirani na husindikiza magari ya wafanyabiashara yenye sukari ili kupita kwenye vizuizi vya barabarani kirahisi.

 “Wanapigiana hadi simu kutaarifiana, kwamba jamani eee kuna gari lenye namba fulani linakuja na mzigo, likifika hapo lipite bila matatizo.

 Wanafanya hivi kwa maslahi yao binafsi na si kuwasaidia Watanzania. “Nimemwagiza RPC (Kamanda wa Polisi wa Mkoa) na kundi lake, lakini pia nimemwagiza Kaimu Mkuu wa Mkoa (Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Geofrey Ngatuni) kukomesha suala hili haraka.

 Kama itaonekana wanashindwa, basi tutawaagiza Jeshi (JWTZ) kuingia kati ili kudhibiti. “Hatutaki kufika huko, nawaomba polisi wafanye kazi yao ipasavyo ili kukomesha hali hiyo mara moja,” alisema Pinda.
source Habari Leo

No comments:

Post a Comment