Pages

September 21, 2011

Kulikuwa na sababu shauri hili kufika hapa????

Mahita alipa mil. 12/- fidia ya mtoto

MKUU wa Jeshi la Polisi mstaafu (IGP), Omar Mahita, amesalimu amri ya mahakama ya Kinondoni baada ya jana kutoa sh milioni 9 kati ya milioni 12 alizoamriwa kulipa kwa ajili ya fidia ya malezi ya mtoto aliyezaa na msichana wake wa kazi ambaye awali alimkana mahakamani.

 Mahita alilipa fedha hizo jana kupitia kwa wakili Charles Semgalawe na kutoa ahadi ya kumalizia kiasi cha sh milioni 3 zilizosalia ndani ya siku 30. Malipo hayo yanafuatiliwa na kampuni ya udalali ya Nasm Auction Mart.

 Awali kabla ya Mahita kulipa fedha hizo, alipewa siku 14 zilizomalizika jana baada ya mlalamikaji Rehema Shabani ambaye ni mama mzazi wa mtoto Juma Omar Mahita kwenda kudai mahakamani fidia kutokana na mdaiwa huyo kuchelewesha malipo aliyoamriwa na mahakama.

 Katika kesi ya msingi, mahakama ilimpa ushindi mlalamikaji Rehema kwa kumtambua mtoto Juma kuwa ni mtoto halali IGP Mahita.

 Katika hukumu hiyo mahakama ilimtaka Mahita mbali na kumtambua mtoto huyo kuwa ni wake pia ilimuagiza kulipa sh 100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo.

 Mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mahita alipinga na kuamua kukata rufaa mahakamani akidai hukumu iliyotolewa na mahakama ya Kinondoni si halali, lakini mahakama hiyo iliyatupilia mbali maombi hayo.

 Kwa sasa mtoto wa Mahita Juma Omar anasoma kidato cha kwanza katika sekondari ya Hananasif iliyoko Kinondoni.

No comments:

Post a Comment