Pages

October 20, 2010

Mwalimu Nyerere for sale

Just back from Lindi and Mtwara,
Kweli kutembea ni shule kubwa sana, nimeona na kujifunza mengi lakini zaidi ni sanaa ya mawe,
Sanamu hii ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ni jiwe lililochongwa, hakuna sementi wala kuunga kwa namna yoyote, ni jiwe lenye urefu wa mita tatu na ushee, kazi ya Mzee Zeno wa kijiji cha Mwena, (nitaandika habari na kazi zake zaidi hapa hapa)
Kikubwa ni kwamba sanamu hii inauzwa, najua wapo wapenzi wengi wa Mwalimu, kama Mzee Sabodo, nakumbuka alivyokuwa anaangaikia na ile sanamu pale Mwenge, bila wanapenda kuona na pengine kununua sanamu hii,
Zaidi ni kuwa mzee huyu anaweza kuchoga sura yako katika jiwe na kubaki na kumbukumbu ya kudumu.
Kweli tembea uone.

No comments:

Post a Comment