Pages

August 25, 2009

Mishahara ya Waheshimiwa JUU

SERIKALI imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia mwezi Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7

Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu. Kwa kifupi tu; Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/= Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/= Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/= jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/= jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/= Kwa hali hii kweli tutapona? Source:Mwananchi

No comments:

Post a Comment