Pages
▼
August 25, 2009
Mazishi ya Wanafunzi 12 yanafanyika leo
Mazishi ya Wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodo mkoani Iringa waliofariki kwa ajali mbaya ya moto Bwenini yanafanyoka leo hii hapo shuleni katika kaburi la pamoja.
Wanafunzi waliokufa katika tukio hilo ambalo leo watazikwa kaburi moja ni ni Matrida Mtewele, Adelvina Kwama na Elizaberth Mtavila ambao walikuwa wanasoma kidato cha kwanza.Wengine ni Digna Nduguru, Chake Kuyaa, Seciliana John, Lazia Kihwele, Witness Mbilinyi na Stellah Mwigavilo waliokuwa wanasoma kidato cha pili.Pia wamo Falha Abdallah na Jesca Wissa waliokuwa kidato cha tatu na Maria Ndole wa kidato cha nne ambapo alisema kutokana na marehemu hao kuteketea kiasi cha kutotambulika, wametumia njia zingine kupata majina yao
Imebidi miili hii izikwe kwa pamoja kutokana na zoezi la kutambua miili hiyo kuwa gumu kutoka na kuungua vibaya.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
Picha za Mazishi zitafuta si muda.
Picha kwa hisani ya Fransis Godwini
No comments:
Post a Comment