Pages

March 30, 2009

RIP Hamidu Bisanga

Mazishi ya Marehemu Hamidu Bisanga (59) mwandishi wa habari wa siku nyingi aliyefariki dunia jana kwa ajali ya gari katika eneo la Kijitonyama karibu na Millenium Tower yanatarajiwa kufanyika kesho ktk makaburi ya Kisutu. Katika Uhai wake, Bisanga alifanya kazi kama Mhakiki wa lugha katika kiwanda cha Printpak mwaka 1973 hadi 1975 na baadaye katika Magazeti la Serikali ya SundayNews na DailyNews kuanzia mwaka 1975 hadi 1990 akiwa mwandishi wa habari na baadaye mwaka 1990 hadi 1994 alifanya kazi katika magazeti hayo akiwa Msanifu Mkuu.

Mwaka 1994 hadi 1998 aliajiliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kama Afisa uhusiano na mwaka 1998 aliajiliwa na Shirika la Maendeleo (NDC) akiwa Meneja uhusiano hadi August mwaka jana alipohamia katika Kampuni ya BayPort kuwa Meneja Uhusiano na Masoko.

Pia Marehemu Bisanga aliishawahi gazeti la African, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC),Sauti ya America na wakala wa Habari wa Ufaransa.

No comments:

Post a Comment