Pages

March 30, 2009

Saba wathibitika kufa ajali ya treni Dom.

MAITI za watu waliokufa katika ajali ya treni iliyotokea katika kitongoji cha Pandambili, katikakati ya stesheni ya Gulwe na Igandu hazijatambuliwa hadi kufikia hii leo.
Kulingana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma , William Lukuvi jumla ya watu saba ndio waliofariki katika ajali hiyo na wengine saba kujeruhiwa.
Lukuvi alisema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma ambapo maiti hizo zimeshindwa kutambuliwa kutokana na majina yaliyoandikwa katika tiketi zao kutokamilika..

No comments:

Post a Comment