Pages

March 28, 2009

Kilwa Road "mukide"

Barabara ya Kilwa yaelekea kukamilika hivyo kupunguza (au kuongeza) usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii hasa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake.
Pamoja na juhudi na nia njema za serikali kutengeneza miuondo mbinu ya jiji letu hili ambazo hazina budi kupongezwa lakini nna pata mashaka na maafisa mipango wetu (Kama kweli tunao) jinsi au namna ya vile miradi hii ambavyo anapangwa au kutekelezwa.
Hebu tuangalie barabara hii na ile ya Mandela jinsi vile zajengwa leo hii, mi nadhani dizaini hii ni ya miaka ya 70 na si elfu mbili na ushee kwani sidhani kuwa kwa msongamano huu unaokua kila uchao bado twaitaji barabara za njia nne zisizozingatia watumiaji wengine mbali na wa vyombo vya moto.
Barabara zote hizi hazina njia ya waendesha baiskeli yaani haipashwi kuchanganya baiskeli na waenda kwa miguu bali kila mmoja awe na njia yake, nadhani yawezekana Bongo ndo sehemu hatari zaidi kwa watumiao ingini kiuno kuliko sehemu zinginezo, na kwakweli usafiri huu bado wafaa na watumika sana nchi za wenzetu zilizoendelea mpaka leo hii kama picha hizi hapa zioneshavyo.

No comments:

Post a Comment