Pages

March 27, 2009

JK achekecha Ma DC

  • Saba wastaafishwa,

  • 15 waingia,

  • 54 wahamishwa,

  • 2 kiporo

  • Ngulume, Mashimba, Maarugu, Dololo, Holela, Madaha nje

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya kwa kuteua wapya 15, kustaafisha saba na kuwabadilisha vituo 54.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), ilionyesha pia kuwa wakuu wa wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameondolewa baada ya hivi karibuni kuteuliwa kuongoza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wakuu wapya na wilaya zao kwenye mabano ni Mercy Silla (Arumeru), Norman Sigalla (Hai), Kanali Issa Njiku (Misenyi), Angelina Mabula (Karagwe), Dk. Rehema Nchimbi (Newala), Francis Isaac (Mbulu), Luteni Kanali Benedict Kitenga (Rorya) na Luteni Kanali Cosmas Kayombo (Mbarali).

Wengine ni Christopher Kangoye (Kwimba), Queen Mlozi (Ukerewe), Fatuma Mwassa (Mvomero), Fatma Ally (Nanyumbu), Juma Madaha (Tunduru), Anatory Choya (Kishapu) na Erasto Sima (Korogwe).

Zaidi tembelea hapa

No comments:

Post a Comment