Pages

February 19, 2009

Liyumba atoweka????????

Wadhamini wa mshitakiwa Amatus Liyumba, Benjamin Nguluguni (kushoto) na Otto Agaton, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo baada ya kukamatwa kwa kukosekana mshtakiwa Liyumba.
DHAMANA aliyopewa Amatus Liyumba imeingia dosari baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa pamoja na wadhamini wake, lakini juzi na jana alisakwa na maafisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) lakini hakuonekana.

Alitakiwa apandishwe mahakamani jana, lakini badala yake maafisa wa takukuru waliambulia kuwakamata wadhamini na wakakiri mahakamani hapo kuwa Liyumba haonekani. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ilitoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba ikiwa ni siku moja tu baada ya kupewa dhamana na mahakama hiyo katika mazingira ambayo hayakuwaridhisha upande wa mashitaka. Hakimu Hadija Msongo jana alikiri kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamtwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake. Hata hivyo hakueleza sababu ya mahakama kutoa hati hiyo kwa kile alichodai kuwa jalada la kesi hiyo tayari limepelekwa mahakama kuu. Ifate hapa baadaye.

No comments:

Post a Comment