Pages

February 19, 2009

Dk Kitine: AZOZA.

Dk Kitine: Nchi iko hatarini

MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Makete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), katika serikali ya awamu ya tatu, Dk Hassy Kitine ameonya kwamba, uchafu na wizi mkubwa wa rasilimali za taifa, mustakabali mbaya wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi vinavyoikabili nchi, vinahatarisha usalama wa taifa.

Kauli ya Dk Kitine ambaye alishika wadhifa huo wa Ukurugenzi katikaIdara ya Usalama wa Taifa, wakati serikali ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imetolewa wakati nchi ikiwa imegubikwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya ufisadi na vita ya chini kwa chini ya kugombea madaraka.

Akizungumza katika mkutano maalumu na baadhi ya vyombo vya habari katika mgahawa wa Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana, Dk Kitine alionya kwamba, uchumi na maliasili za taifa zimeshikwa na wageni, huku Watanzania walio wengi wakifanya kazi za udereva, ufagiaji barabarani, kazi za ndani na mashambani. "Nimewaiteni kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu, kama mnavyofahamu mimi nimeshika nafasi mbalimbali nyeti kuanzia wakati wa Mwalimu," alifahamisha. ICHEKI HAPA.

1 comment:

  1. Amezungumza ya maana kuliko nilivyowahi kusikia la maana lolote katika siasa za Tanzania baada ya Nyerere J. Kambarage. Tatizo ni kuwa hao wanaozungumziwa hawataona ukweli huu bali watajitahidi sana kupinga na kupuuzia maonyo haya kama vile hayawahusu, na hapo ndipo chanzo cha kutokufika kokote katika hatua za kimaendeleo. Sijui tuna viongozi wenye ubongo wa aina gani.

    ReplyDelete