JUKWAA la Wahariri Co Limited limetangaza kumfungulia Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni George Mkuchika baada ya kugoma kuandika habari zake kwa takribani miezi minne sasa.
“Tayari gazeti liko mitaani, tunatangaza kumfungulia Mkuchuka. Lakini pia tunalaani kitendo cha kutumia sheria mbovu kuvifungia vyombo vya habari,” alisema mwenyekiti wa jukwaa hilo Sakina Datoo. Hata hivyo jukwaa hilo lilikishambulia kituo cha televisheni cha ITV kuwa kilifikia hatua ya kurusha habari za waziri huyo hasa baada ya Mkuchika mwenyewe kuzungumzia habari zinamlinda mmiliki wa kituo hicho Reginald Mengi.
No comments:
Post a Comment