Pages

January 26, 2009

Ujumbe kila kona..

Huwa nina kawaida au tabia ya kusoma kila kilichombele yangu kilichoandikwa, sijui kama kawaida/tabia hii ni mzuri au la kila mtu aweza sema lake.

Lakini jambo moja nilijualo ni kuwa kila nisomapo chochote kile sikosi kupata ujumbe au kujifunza jambo,

Ni wangapi wetu uwa twapoteza japo sekunde ka si dakika kusoma hivi vitiketi vya daladala? hebu soma kwa makini tiketi hii alafu niambie kile ulichogundua au kujifunza hapo. Jibu unalo.

Leo nimebahatika kupanda magari mawili ambalo kila moja lilikuwa na jumbe toka pande mbili za imani zetu kuu au kielelezo cha ustaarabu na utamaduni wetu watanzania wa kuweza kujichanganya pasipo kuwa na mikwaruzano na kila mtu akashika hamsini zake.

Moja wapo ni hili lililonipa tiketi hiyo, na la pili lilikuwa na kila namna ya ujumbe ndani ya basi wa Qorani takatifu kuanzia ule wa "Allah is One" N.K Lakini muziki uliokuwa ukitutumbuiza na kutusahaulisha machungu ya foleni za jiji la Bongo ulikuwa toka kwa Dada Upendo Nkone, kwa wale wapenzi wa nyimbo za Gospel mwajua ni nyimbo za aina gani dada huyu aimba au za milindimo ya namna ipi. Basi ilikuwa ni burudani kwetu sote, na hii ndio Tanzania kisiwa cha amani na ustaamilivu wa imani.

Na kwa wale wasiotaka kuokoka someni ujumbe huo.

No comments:

Post a Comment