Pages

January 27, 2009

JE PICHA HUSOMAYO GAZETINI NDIVYO ILIVYOPIGWA?

Origino picha
Origno picha

Tumekuwa na ugomvi mkubwa sana na rafiki zangu watengeneza kurasa au graphic designer juu ya namna wanavyozitengeza au kuharibu katika kutengeza picha kabla ya kuchapishwa gazetini.

Hapo juu ni mifano michache tu ya jinsi gani mpiga picha waweza kuonekana bomu kwa msomaji kumbe kuna mtu mwingine ambaye hajulikani kwa msomaji ndo aliosababisha.

Mfano mmoja mdogo ni picha ya chini ofisi za ndege pale JNIA Dar, picha hii ilipigwa siku moja baada ya ATCL kuanza tene safari za ndani ya nchi huku wakiruka na abiria mmoja au wanne kwa ndege ya abiria 50, hali halisi yaonesha katika picha hii ni kwa jinsi gani pana kafoleni kadogo ktk Ofisi za PW lakini hakuna hata mmoja ATCL, lengo la picha hii ni kujaribu kuyaweka maneno au habari hii katika picha na ndivyo ilivyokabidhiwa na maelezo kama hayo.

Lakini jambo la kushangaza kesho yake picha ilitika kama ilivyo na maelezo tofauti na yale ya mpigapicha au hata habari yenyewe, jambo hili ni la kusikitisha sana, kwani mpigapicha anaonekana muongo sababu ya mtu mmoja tu.

WADAU WANA FANI MNA MAONI GANI? NITUMIE MIFANO ULIYONAYO TUIWEKE HEWANI ILI KUAMSHA MJADALA WA NINI KIFANYIKE.

2 comments:

  1. Mpiga picga au mwandishi wa habari anapopiga picha au kuandika stori anakuwa na lengo na mtazamo fulani kuhusu picha au stori husika.
    Mhariri na watu wa Graphic mara zote wakao kwenye eneo la tukio. Hivyo, hutafsiri picha au stori kutokana na mtazamo wao wenyewe.
    Ushauri: Ni suala ambalo unaweza kuliweka wazi katika vikao vyenu vya ndani kwamba mpiga picha au mwandishi wa stori akashirikikishwa katika kuandaa au akawa na uamuzi wa jinsi picha au stori au picha yake itoke.
    Ni kazi ya ziada, lakini kwa wale walio makini na kazi zao, ni jambo la muhimu.
    Mdau
    Faustine

    ReplyDelete
  2. Anonymous2:20 PM GMT+3

    Mi naona hapa kuna kosa au mkosa zaidi ya Graphic Designer. Nasema hivyo kwa sababu, kama maelezo yako ya Caption yalikuwa yanahusu foleni au uhaba wa foleni inakuwa ngumu kwake kuelewa ulikusudia nini hasa. Ila mhariri wa hiyo kurasa pia ameshindwa kutambua lengo lako pia lilikuwa nini. Hivyo mi nafikili lawama zinaenda zaidi kwa Sub-Editor yeye ndo alitakiwa kumuongoza Graphic Designer kuwa lengo hapa lilikuwa hili na si hili.
    Ushauri wangu: Nadhani caption ziandikwe kwenye file info ya picha (Photoshop fileinfo) kabisa kuliko kuandikwa kwenye text editor zikiwa nyingi mpaka kusababisha wakati mwingine kuchanganya caption.
    Mdau, Kimox
    http://kimox.blogspot.com

    ReplyDelete