Pages

January 26, 2009

Mpiganaji Athumani aendelea vyema.

Mpiganaji Athumani Khamis akijuliwa khari na Maofisa toka TSN, Mkumbwa Ali Naibu Mhariri Mkuu na Emmanuel Makene Katibu wa shirika katika Hospital ya Millpark huko Afrika Kusini katika jiji la Jo'burg hivi karibuni.

Khali ya Athumani inaendelea vizuri na inatia matumaini, kwani hivi sasa angalau ameanza kupata hisia miguuni na kuweza kuinua mikono ni jambo la kumshukuru Mungu sana na hakika kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu muumba wa vitu vyote nina imani kubwa kuwa siku moja Mpiganaji huyu atakuja tembea tena kwa miguu yake kwani hakuna neno gumu lakumshinda MUNGU.

Blogu hii inakuombea sana Mpiganaji upone haraka na upate kurudia maisha yako kama zamani na hali hii iwe kwako sehemu ya historia tu.

No comments:

Post a Comment