Pages

January 11, 2009

BURIAN CASSIAN MALIMA..

Kesho tunataria kumuaga rasmi Cassian Malima kabla ya kusafirishwa kuelekea Musoma kwa safari yake ya mwisho hapa Duniani ambapo kila mwanadamu aliyezariwa na mwanamke basi ni lazima ataipitia.

Sidhani kama naweza andika vyema tanzia ya Marehemu Malima, lakini itoshe kusema tu kuwa kwa kipindi kifupi sana nilichfanyakazi naye basi yapo mengi mno ya kujifunza toka bosi wangu huyu ambaye kwa hakika sina wa kumfananisha naye kwa sasa.

Wakti najiunga na TSN nakumbuka ndiye aliyekuwa Mhariri Habari pale, kwa kweli ni kiongozi astahilie kuigwa kwa namna ambavyo alikuwa akituongoza katika idara ile ya habari wakti huo tuna gazeti moja tu, alifanya wengi wetu tuliojiunga kwa pamoja au kwa akukalibiana tujisikie amani sana kufanya kazi TSN kwa jinsi ambavyo alikuwa akongoza kitengo chake hicho kwa ushirikiano mkubwa na wote waliochini yake, nakumbuka wakti naishi Bgrn alikuwa akinipigia simu mara gari limfuatapo kuja kazini ili wanipitie lakini hata palipokuwa na tatizo alikujulisha kwa simu yake ili usipate tabu kusubiri, ni nani sasa hivi aweza fanya hivyo?

Hakuwa mwepesi wa hasira na ata ulipomkasirisha kikazi atakuita atakuonya na itaishia hapo hakuwa na kisasi hata kidogo mtani wangu huyu, kwa kweli sidhani kama naweza mwelezea hapa pakatosha au nikamaliza kile ambacho nalitaka kueleza lakini itoshe kusema kuwa TSN tumeondokewa na mtu muhimu sana si kwa sababu hatunaye tena ndo maana naweza sema haya la hasha, bali haya tumekuwa tukiyangoea sana na baadhi ya wanaTSN wanajua juu ya hili.

Malima alikuwa rafiki wa kila mtu na hakuwa wa kujipendekeza wala kujikomba alipendana na kila mtu si mkubwa wala mdogo waulize waandishi waliofanya kazi naye, madereva, madereva, matarishi na hata wakubwa zetu pia, hakika tumepoteza rafiki, ndugu na mtani.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA CASSIAN MALIMA

No comments:

Post a Comment