Rais Yoweri Museven wa Uganda (wapili kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kutafuta suluhu ya Mgogoro kati ya Serikali ya Burundi inayoongwanzwa na Rais Pierre Nkurunziza (watatu kushoto) na Kikundi cha The Palipehutu National Liberation Front (FNL) kinachoongozwa na Agathon Rwasa, akizungumza katika mkutano wa kutia saini makubaliano ya kumaliza mgogoro huo, mjini Bujumbura Desemba 4, 2008. Kushoto ni Rais wa Zambia, Rupiah Banda na kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo. Wapili kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya, Kalonzo Musokya.
Rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza (kushoto) na Kiongozi wa Kikundi cha wapiganaji cha The Palipehutu National Lineration Front (FNL), Agathon Rwasa wakitia saini makubaliano ya kuacha mapigano katika mkutano wa Usuluhishi ulioongozwa na mwenyekiti wa kamati ya kusuluhisha mgogoro huo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, mjini Bujumbura, December 4, 2008.
No comments:
Post a Comment