Pages
▼
August 8, 2008
JIMY ELIAS AFARIKI
Mwandishi wa siku nyingi Jimmy Elias afariki
MWANDISHI wa habari wa siku nyingi, Bw. Jimmy Elias (41) amefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam, baada kuugua kwa takribani mwezi mmoja.
Mmoja wa ndugu wa marehemu, Bw. Richard Mwaikenda, alisema Jimmy (pichani) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo na alikuwa akiendelea na matibabu nyumbani lakini alipozidiwa alipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.
Mwili wa marehemu unatarajia kuagwa KESHO mchana saa sita nyumbani kwake Kiwalani Bombom na baadaye kusafirishwa kuelekea katika kijiji alipozaliwa Ngana, wilayani Rungwe mkoani Mbeya tayari kwa mazishi yatakayofanyika Jumapili.
Hadi mauti yanamkuta alikuwa Meneja Mauzo wa gazeti la Ngurumo za Simba na jarida la StarSport tangu yalipoanzishwa.pia katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuandikia magazeti ya Dar Leo (zamani Majira Jioni) na Mfanyakazi.
Ameacha mke Bi. Mary Katendele na watoto watatu ambao ni Boniface, Jackson na Staford.Katika uhai wake alikuwa mpezi mkubwa wa mpira wa miguu ambapo alikuwa ni mwanachama hai wa Klabu ya Simba.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
No comments:
Post a Comment