August 8, 2008
JIMY ELIAS AFARIKI
Mwandishi wa siku nyingi Jimmy Elias afariki
MWANDISHI wa habari wa siku nyingi, Bw. Jimmy Elias (41) amefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam, baada kuugua kwa takribani mwezi mmoja.
Mmoja wa ndugu wa marehemu, Bw. Richard Mwaikenda, alisema Jimmy (pichani) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo na alikuwa akiendelea na matibabu nyumbani lakini alipozidiwa alipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.
Mwili wa marehemu unatarajia kuagwa KESHO mchana saa sita nyumbani kwake Kiwalani Bombom na baadaye kusafirishwa kuelekea katika kijiji alipozaliwa Ngana, wilayani Rungwe mkoani Mbeya tayari kwa mazishi yatakayofanyika Jumapili.
Hadi mauti yanamkuta alikuwa Meneja Mauzo wa gazeti la Ngurumo za Simba na jarida la StarSport tangu yalipoanzishwa.pia katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuandikia magazeti ya Dar Leo (zamani Majira Jioni) na Mfanyakazi.
Ameacha mke Bi. Mary Katendele na watoto watatu ambao ni Boniface, Jackson na Staford.Katika uhai wake alikuwa mpezi mkubwa wa mpira wa miguu ambapo alikuwa ni mwanachama hai wa Klabu ya Simba.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Umati wa watu unaozidi kufurika huko Loliondo kwa dhumuni moja tu, kupata dawa ambayo inaaminika inatibu magonjwa sugu ama yaliyoshin...
-
The Edmark Double Bonus Marketing Plan consists of both the Point Sharing System and the Block System. Thus, giving maximum benefits ...
-
Alert over Kenya's first case of H1N1 flu Minister for Public Health and Sanitation Beth Mugo addresses the media in Nairobi. Kenya...
-
Uongozi wa Shule za Marian Bagamoyo unawakaribisha wote kwenye Fundraising Dinner hii ili kuchangisha fedha ya Kujenga na kue...
-
Bernard Madoff gets maximum 150 years in prison NEW YORK – Convicted swindler Bernard Madoff was sentenced to 150 years in prison Monda...
-
Mshindi wa Kiti cha Urais Zambia, Michael Sata. Jubilation and dance characterised the streets of Lusaka , the country’s capital...
-
August 13-16th, 2009 in Nairobi, Kenya. Kelele is an annual African bloggers’ conference held in a different African city each year and ru...
-
WINNERS Boulevard.: Biashara ya Masoko ya Mtandao : Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni a...
-
Porn image ban sparks concern A new law, slated to come into force in January, will make the possession of images deemed to be of an extre...
No comments:
Post a Comment