Pages

April 23, 2008

TBL NA WAJANE

Ofisa Tarafa ya Ilala, Bw. Suleiman Mwenda. akimkabidhi mmoja wa wanachama wa kikundi cha Wanawake Wajane cha The Good News Social Welfare Organisation (GOSOWO), Bibi Haruna Shamte cheti cha kuhitimu mafunzo ya kudarizi nguo pamoja na kutengeneza batiki yaliyogharamiwa hivi karibuni na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wanaoshuhudia hafla hiyo iliyofanyika Vingunguti, Dar es Salaam jana, ambapo pia TBL iliwakabidhi msaada wa vyerehani vyenye thamani ya sh. milioni 4 ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Bi. Dorris Malulu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa GOSOWO, Bw. Frank Mshahara.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Dorris Malulu akifurahia kuona kitenge cha batiki chenye jina la kampuni hiyo baada ya kukabidhiwa zawadi na Kikundi cha Wanawake Wajane cha The Good News Social Welfare Organisation (GOSOWO), baada ya kukipatia msaada wa vyerehani vya thamani ya sh. milioni 4 pamoja na kuwagharamia sh. milioni 1.5 za mafunzo ya kudarizi na kutengeneza nguo za batiki. Kulia ni Ofisa Tarafa ya Ilala, Bw. Suleiman Mwenda

No comments:

Post a Comment