Pages

April 21, 2008

Atimaye Chenge abwaga manyanga.

Rais akubali kujiuzulu kwa Chenge Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo April 20, 2008, amepokea barua kutoka kwa Waziri wa Miundo Mbinu, Mheshimiwa Andrew Chenge ya kujiuzulu wadhifa wake na Rais amekubali ombi hilo la kujiuzulu. Rais ameuelezea uamuzi huo wa Mhe Chenge kama uamuzi wa busara kwa kutilia maanani mazingira ya sasa. Katika barua yake kwa Rais, Mhe Chenge amesema kuwa pamoja na kwamba shutuma dhidi yake bado zinachunguzwa, mapenzi yake kwa nchi na chama chake, yamemsukuma kujiweka pembeni. Mhe Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi. Mwisho Imetolewa na Ikulu, 20th April, 2008

No comments:

Post a Comment