Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael
Shirima (kulia) akitoa tamko rasmi kuhusiana na mpango wa Uuzaji wa Hisa katika
Soko la Awali (IPO) utakaoanza tarehe 7 – 28 Oktoba, 2011 wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar, Katikati ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja
Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akifuatiwa na Meneja Uhusiano wa
Wateja katika Benki ya Stanbic Bi. Naomi Vincent.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam Oktoba 4, 2011.
Bodi
ya Wakurugenzi wa shirika la ndege la Precision Air Services Plc inapenda
kuwataarifu kwamba mpango wetu wa Uuzaji wa Hisa katika Soko la Awali (IPO) na
kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) imepatiwa vibali vyote
husika na sasa ipo tayari kwa hatua zinazofuata.
Kilichoidhinishwa
ni ratiba ya matukio ya utaratibu mzima wa mchakato huu:
Kampuni
itatoa jumla ya hisa 58,841,750 kwa ajili ya ununuzi kwa bei ya 475 kwa kila
hisa. Huku idadi ya chini ya kuanza kununua hisa ambayo mtu ataruhusiwa kununua
itakuwa ni hisa 200.
Nakala
ya waraka wa matarajio ya kampuni ambayo pamoja na mambo mengine, maelezo
maalumu ya ufafanuzi na ununuzi wa hisa zinapatikana katika tovuti ya Precision
Air www.precisionairtz.com
tarehe 4 Oktoba 2011.
Kwa
niaba ya Wakurugenzi ya Bodi, utawala na wafanyakazi wote napenda kutoa
shukurani zangu za dhati kwa wateja wetu kwa mchango wao na ushirikiano
yakinifu ulioweza kufanikisha maendeleo na ukuaji wa shirika la ndege hili
tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.
Michael N
Shirima
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
|
Pages
▼
No comments:
Post a Comment