Pages

October 4, 2011

LINI KUTAKUWA NA MAHUSIANO AU UTARATIBU MZURI WA KAZI NA HAWA JAMAA ZETU??????????


Ni lini hawa ndugu zetu watatambua umuhimu wa kazi ya kila mmoja wetu? haya ni matukio ambayo yamekuwa yakijirudia kila mara ya ndugu zetu wa usalama kuona kazi za watu wengine si tija kwao. 


Japo wana jukumu kubwa la kuangalia usalama wa viongozi wetu lakini ni vyema wanapokuwa wanafanya mpango wa usalama kifikiria pia kuwa katika matukio hayo hawatakuwa peke yao, wanashindwa nini kuwahusisha wadau wengine kama watu wa habari na hasa wapiga picha juu ya namna nzuri kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi zaidi pasipo kubugudhiana bila sababu kama hivi?


Ikulu yetu inahitaji mtu anayeitwa Visual Director ambaye anakuwa kiunganishi cha watu wa usalama na waandishi ama wapiga picha, huyu ni mpiga picha lakini zaidi ya mpiga picha anayeweza kutambua na kuelekeza mazingira mazuri ya wapi wapiga picha wanaweza kukaa na kupata picha vizuri pasipo kusukumana na kunyanganyana vifaa vya kazi kama inavyoonekana hapa. 


Wapo viongozi wa nchi mbalimbali wamepata kututembelea wapo waliokuwa na watu kama hao, nina uhakika makachero wanawafahamu na wameshakutana nao, kwa kawaida utangulia siku kadhaa eneo la tukio kuweka mazingira mazuri ya kazi. 





KAMANDA WA MATUKIO: MAKACHERO WA KIBONGO WAWANYANYASA WAPIGA PICHA ZA ...: Maofisa wa usalama wa Taifa wakiwa wamemnyang'anya kamera na kumtoa eneo lake la kazi Mpigapicha wa magazeti ya The Guardian na Nipashe, K...

No comments:

Post a Comment