Pages

September 12, 2011

Zanzibar - Mamia bado hawajulikani walipo


  • Miili 240 yapatikana 
  • 39 wazikwa na serikali
  • Helcopter, Wazamiaji na Boti za uokozi zaendelea na juhudi za uokoaji



Add caption
MJI wa Zanzibar na viunga vyake, jana uliendelea kuwa katika taharuki na simanzi kubwa kutokana na baadhi ya familia kuwakosa ndugu zao waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Spices  Islander ambayo ilipinduka, kisha kuzama katika eneo la Nungwi kati ya Visiwa vya Unguja na Pemba.Wakati familia kadhaa zikisubiri majaliwa ya ndugu zao wanaoaminika kwamba walikuwa kwenye meli hiyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), jana ilitangaza kwamba waliopoteza maisha ni watu 197 na kwamba watu 619 wameokolewa wakiwa hai.

 Taarifa hiyo ya SMZ iliyotolewa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed inathibitisha kwamba meli ya MV Spices Islander ilikuwa na zaidi ya abiria 610 ambao ni uwezo wake. Kwa takwimu za waziri huyo, imethibitika kwamba ilikuwa imebeba abiria 816.

 Rais Jakaya Kikwete jana aliwatembelea wakazi wa Nungwi kuwapa pole kwa msiba huo mkubwa kwa taifa na kwa mujibu wa Waziri Aboud, mkuu huyo wa nchi alitarajiwa pia kuongoza kikao cha Baraza la Taifa la Ulinzi na Usalama kujadili maafa hayo.

 Kadhalika, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal pia aliwatembelea wakazi wa Nungwi na pia kuwapa pole wafiwa na walionusurika katika ajali hiyo mbaya.
 

Aboud alisema kati ya waliokufa, 158 walitambuliwa na kuzikwa na jamaa zao wakati maiti 39 hawakutambuliwa hivyo kuzikwa na Serikali katika eneo la Kama, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

 Alisema Serikali pia imeandaa makaburi mengine 134 kusubiri maiti ambao wanaendelea kuokolewa kutoka baharini.
 

Alisema SMZ imewasiliana na wakuu wa Mikoa ya Tanga, Pemba na Mombasa ili wasaidie upatikanaji wa maiti ikiwa wataonekana katika fukwe za maeneo hayo. “Kesho jioni (leo) tutakuwa na swala ya pamoja kwa ajili ya kuwatakia heri ndugu zetu,” alisema Aboud.

source: Mwananchi 

No comments:

Post a Comment