Askofu Mkuu
wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, amesema haungi mkono
shule za sekondari za kata nchini kwa sababu hazijaandaliwa vizuri kuwawezesha
watoto kukomaa na kupata elimu iliyo bora.
Aliyasema
hayo jana katika mahubiri yake kwenye kanisa kuu la Anglikana Mbeya ikiwa ni
siku ya mwisho ya ziara yake ya kutembelea Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini ya
kanisa hilo.Dk. Mokiwa
alisema shule nyingi za kata zimejengwa kisiasa na ndiyo maana hata elimu
inayotolewa katika shule hizo haikidhi mahitaji ya ushindani wa kielimu.
Alisema
kutokana na shule hizo kujengwa kwa manufaa ya kisiasa, wanafunzi wake wamekuwa
wakisoma kwa mtindo wa kinadharia na kukaririshwa, alisema hali ambayo
haimfanyi mwanafunzi kuelewa vizuri.“Vijana wa
siku hizi mnafundishwa maswali yote mnapewa majibu ya kuchagua, mnapofundishwa
suala la ufahamu mnashindwa kuelewa,” alisema Dk. Mokiwa.
Askofu Dk.
Mokiwa alisema ili kurudisha elimu katika kiwango bora, serikali irejeshe shule
za zilizokuwa zikimilikiwa na taasisi za
dini ili wao waziendeleze kwa sababu shule hizo zilimjenga mwanafunzi kiroho na
kiakili.
Alisema
serikali ilizichukua shule hizo kama
majengo na kuacha msingi ambao ulikuwa umewekwa na shule hizo ambao ulikuwa na
mfumo mzuri wa ufundishaji uliozingatia maadili ya mwalimu na mwanafunzi.“Shule za
misheni zirudi ni mali ya kanisa, na zitarudi zenyewe au kwa kurudishwa na
waliozichukua,” alisisitiza Dk. Mokiwa.
Akizungumzia
suala la ufisadi, Dk. Mokiwa alisema ufisadi ni roho na tabia mbaya ambayo ipo
katika kada mbalimbali kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa.
Alisema
ufisadi unapaswa kukemewa kuanzia ngazi ya familia kwani ikiachwa baadaye unaharibu taifa katika sekta za
bararabara na umeme na hivyo kuzua malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment