Pages

September 14, 2011

Miaka 5 sasa.


Miaka mitano ni michache sana kwa mwanadamu, ni umri ambao mtoto kama atakuwa ameenda vyema basi atakuwa chekechea ambapo atatarajia kukaa ama mwaka au miaka miwili kabla ya kwenda shule ya msingi, huyu ni mtoto bado, lakini kwa Shirika, kampuni, biashara, na hata blog si umri mdogo huo, ni mkubwa.

 Ni umri mkubwa kwa bloga kama ilivyo kwa kampuni, Shirika, ama nchi, ingekuwa ni urais iki ni kipindi ambacho ama rais anamaliza muhula wa kwanza au wapili na hivyo kuhitaji ufanyike uchaguzi ili apatikane mwingine, hivyo si muda mchache hata kidogo.

 
Kwa blog kufika muda huu ikiwa hai na bado iko ewani si kazi ndogo, ebu fikiria ni vitufe (keyboards) ngapi zimegingwa na pengine kuharibika katika juhudi za bloga kurusha ewani kile atakacho wadau wakisome? au ni sikirini ngapi zimemmulika bloga na pengine kutaka kumpofusha ili mradi tu wadau wapate kinachoendela?, au labda ni viti vingapi amekalia, vibanda vingapi (vyaitwa @ café) ameingia na pengine kulazimika kukaa kusubiri muda wake ama kugombana na wahusika kwa kumruka katika foleni ilimradi tu aingie mtandaoni na kuweka blogini kile alicho nacho? je alipotishiwa kufukuzwa kibarua, kisa! kuwajuza wadau.

 Utatambua kuwa si muda mchache hata kidogo, ni mwingi wa kutosha, Bongo Pix Blog kama zilivyo blog nyingine pia imepitia hayo na mengi zaidi ya hayo, lakini ilivuka na sasa inatimiza miaka mitano, shukurani za pekee ziwaendee wadau wote kote ulimwenguni, kwani BPB ina wadau katika mabara yote matano, kinara ikiwa ni Africa, Amerika, Ulaya na Asia.

 Si rahisi kumtaja kila mdau, lakini itoshe kusema kuwa BPB inawashukuru sana nyote, wapo ambao wamekuwa wakichangia, asanteni sana, wapo pia waliokuwa wanapiga simu kutaka kujua kulikoni pale tunapokuwa tumetingwa, nao pia nasema asante, lakini wapo ambao piga uwa lazima wapiti blogini kila siku kuona na kusoma kilichorushwa humo nao nawashukuru lakini shukurani za pekee kwa wewe uliyeamua kuifanya BPB kama favourite yako au home page, wewe ubarikiwe sana.

 Miaka mitano ijayo (panapo majariwa ya Muumba) kutakuwa na mabadiliko makubwa sana, endelea kuitembelea utajionea.
 Asanteni sana Nyote, Bernard Rwebangira,  

1 comment:

  1. Ben, hongera kwa miaka 5 ya kublogu.
    Nakuombea heri na afya njema uendelee kutuelimisha na kutupasha habari kwa njia hii.
    Pongezi jirani!

    ReplyDelete