Pages

September 24, 2011

Hakuna siri tenaaaaa!


Itakuwa vipi unapita mitaa ya Kongo unatungua Jeans yako moja swaaaafi, unaipiga sop sop kisha watinga nayo kitaani, bila kujua kumbe ina kifaa kiduchu maalumu cha mawasiliano ya kidigitali (radio-frequency identification device, RFID), ambacho kinaonesha kila unapoenda, kila mahali ulipo?

 Alafu fikiria waifu anakutwangia, we wamzuga kuwa huko Mbezi, kumbe ye anakuona kupitia mtandaoni kuwa huko chobingo! au waifu kapigilia hiyo jeans wampigia akwambia yuko home kumbe yuko chobingo, kawekwa mtu kati kisawasawa??

 Itakuwa vipi hapo wadau??

 Jibu  kila mtu atakuwa na la kwake, yaweza onekana kama uzushi au mzuka fulani hivi, lakini hapana si mzuka wa uzushi bali ndivyo ilivyo, huko majuu wametengeneza jeans za namna hiyo zijulikanazo kama “Internet of Things” IOT zenye kifaa hicho cha mawasiliano ambacho kinatuma ujumbe mfupi kupitia mtandao wa Twitter kikionesha kila mahali anakopita mvaaji wa nguo.

 Haya ndo mambo ya Teknoligia, itafika mahali bila shaka hatutakuwa na siri au faragha tena, kila kitu kitakuwa hadharani kwa yeyote kuona ama kufuatilia, mmh itakuwa vipi kwa sisi wependa vijizawadi toka majuu, kumbe jamaa anakupa ili aweze kukumonita vyema kila hatua unayofanya, kila unapokwenda, na pengine kila unachozungumza na hao unaozungumza nao?/

 Je hii ni habari njema wadau au mwaonaje? 



It sounds far-fetched, but it's possible - if one of your garments is equipped with a tiny radio-frequency identification device (RFID), your location could be revealed without you knowing about it.

RFIDs are chips that use radio waves to send data to a reader - which in turn can be connected to the web.

This technology is just one of the current ways of allowing physical objects to go online - a concept dubbed the "internet of things", which industry insiders have shortened to IoT. ..

Source: BBC

No comments:

Post a Comment