Pages

September 28, 2011

Elimu kibongo bongo, Migomo kabla ya darasa.

University students display placards as they wait for the outcome of a meeting between their leaders and the Ministry of Education and Vocational Training officials in Dar es Salaam on Tuesday, on their overdue loans which they would have collected on the 27th of this month. (Photo by Robert Okanda)



Elimu ya namna hii kweli tutafika? Elimu ya msingi wasoma kwa taabu, hakuna madawati, vitabu, walimu wa kutosha.

 wafaulu kiMungu Mungu, waenda shule za kata, wakaa gheto kama si kwenda na kurudi zaidi ya kilomita ishirini kwa siku, nako darasani hakuna madawati, hakuna maabara, maktaba hazina vitabu, walimu ni kasheshe. 

Lakini nako wafanikiwa kufaulu kiaina, hatimaye waja chuo, ukidhani kuna unafuu, hali ndo kasheshe zaidi, mkopo hauupati mpaka kwanza muemdeshe mgomo, upigwe virungu na mabomu ya machozi na hii ni kipindi chote mpaka umalizapo kozi yako.



 Muhitimu huyu aliyepitia haya yote mwisho wa siku anakuja kuwa mtu wa namna gani? tunakuwa tumejenga taifa la aina gani kupitia mfumo huo?


 Mimi sijui, wewe je? 

No comments:

Post a Comment