Pages

September 28, 2011

Dowans kulipwa yale mabilioni leo??




KITENDAWILI cha iwapo Kampuni ya kufua umeme ya Dowans inastahili kulipwa tuzo ya Sh94 bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) au la kinatarajiwa kuteguliwa leo wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itakapotoa uamuzi wake wa kisheria.

 Dowans iliwasilisha maombi katika mahakama hiyo ikiomba tuzo ya kiasi hicho cha fedha dhidi ya Tanesco, baada ya kuamriwa na jopo la majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) ya Paris, Ufaransa Novemba mwaka jana.

 Jopo hilo liliketi chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen akisaidiwa na  wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parke na kutoa uamuzi huo wa kuitaka Tanesco ilipe tuzo hiyo ya mabilioni.

 Vyanzo vya habari kutoka Mahakama Kuu, vilidokeza jana kwamba uamuzi wa maombi hayo ya usali wa tuzo hiyo ya Dowans unatarajiwa kutolewa leo.

 Endapo Mahakama Kuu itakubaliana na maombi ya Dowans, basi tuzo hiyo itasajiliwa na kuipa nguvu ya kisheria kulipwa mabilioni hayo.Hata hivyo, Dowans kwa kujihami, imeshafungua maombi mengine ya utekelezaji wa hukumu hiyo ya ICC katika Mahakama Kuu Uingereza kupitia kwa mwanasheria maarufu nchini.

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment