Pages

August 27, 2011

walipa kodi wakubwa Tanzania




Mheshimiwa Spika,
44.         Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:

i.              Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
ii.            National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);
iii.           Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);
iv.            National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);
v.            CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);
vi.           Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);
vii.          Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);
viii.        Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);
ix.           Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);
x.            Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);
xi.           Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);
xii.          Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);
xiii.        Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);
xiv.         Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na
xv.          Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).

From: Hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Dodoma August 26, 2011

Just thinking aloud, 
Kuwa mlipa kodi mkubwa na kushika namba moja ina maana umeingiza mapato mengi pia kwenye biashara uifanyayo na hivyo kulipa kodi stahiki na hatimaye wajikuta umekuwa namba moja, sio, nawaza kwa sauti tu, je inamaanisha nini kwa TBL kuwa kinara?, ni kwamba wameuza sana au niaje? 



Mtu alitarajia yale makampuni yanayojihusisha na vyakula, vinywaji baridi au simu yashike namba kwa naamini yana wateja wengi kuliko tbl, na je yale yanayochimba madini tena mengine yana migodi zaidi ya miwili kanda ya ziwa huko nayo imekuwaje? just thinking aloud!

No comments:

Post a Comment