Pages

August 27, 2011

Pato la Mtanzania, nini maoni yako??

Mineral occurrence in Tanzania by TMAA



UONGEZAJI WA PATO LA MTANZANIA
Mheshimiwa Spika,
46.         Lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ni kuiwezesha Tanzania kuwa na Uchumi wa Kipato cha Kati (Middle Income Country) ifikapo mwaka 2025. Kwa mujibu wa Takwimu za Taasisi ya Taifa ya Takwimu (National Bureau of Statistics) za mwaka 2010; wastani wa Kipato cha Mtanzania kimefikia Dola za Kimarekani 545, sawa na Shilingi 770,464. Hivyo, katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka 15 tunayo changamoto kubwa ya kuongeza kwa kasi kubwa Kipato cha Mtanzania ili kufikia lengo lililokusudiwa la kufikia Dola za Kimarekani 3,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 4.8 kwa mwaka au Shilingi 400,000/= kwa mwezi ifikapo mwaka 2025 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya Uchumi wa Kati.

Mheshimiwa Spika,
47.         Napenda kutumia fursa hii kueleza kidogo kuhusu mwenendo wa takwimu za Mikoa kuhusu kiashiria hiki cha Wastani wa Kipato cha Mwananchi (Regional Per-Capita Income). Mtiririko wa nafasi za Mikoa kwa mwaka 2010 za Wastani wa Kipato cha Mwananchi kwa mwaka ni kama ifuatavyo:

              i.      Dar es Salaam   -           Shilingi 1,740,947
            ii.      Iringa                 -           Shilingi  979,882
           iii.        Arusha               -           Shilingi  945,437
           iv.       Mbeya                -           Shilingi  892,877
            v.       Kilimanjaro        -           Shilingi  879,432
           vi.        Ruvuma              -           Shilingi  866,191
          vii.       Mwanza              -           Shilingi  829,647
        viii.       Manyara              -           Shilingi  772,364
           ix.      Tanga                  -           Shilingi  763,203
            x.      Morogoro            -           Shilingi  744,234
           xi.      Rukwa                -           Shilingi  726,658
          xii.     Mtwara               -           Shilingi  700,436
        xiii.      Lindi                    -           Shilingi  673,096
        xiv.      Mara                   -           Shilingi  642,528
          xv.     Pwani                  -           Shilingi  572,466    
        xvi.     Tabora                -           Shilingi  528,832
       xvii.     Shinyanga        -           Shilingi  510,023
      xviii.     Kigoma              -           Shilingi  499,428
        xix.     Kagera               -           Shilingi  491,713
          xx.     Dodoma             -           Shilingi  485,211
        xxi.      Singida              -           Shilingi  483,922

Mheshimiwa Spika,
48.          Takwimu hizo zinaonesha kuwa Theluthi Moja tu ya Mikoa yote ya Tanzania ndiyo yenye Wastani wa Pato la Mtu ambalo ni juu ya Wastani wa Pato la Mwananchi Kitaifa la mwaka 2010 la Shilingi 770,464. Vilevile, Takwimu hizo zinaonesha kuwa Mikoa Mitano ya mwisho kwa mlinganisho wa Wastani wa Kipato cha Mwananchi ni Shinyanga, Kigoma, Kagera, Dodoma na Singida. Hata hivyo, hali halisi inaonesha kuwa Mikoa hii ina fursa nyingi za kuongeza Mapato kutokana na shughuli mbalimbali za uchumi, na fursa za kibiashara zilizoko lakini Takwimu za Mapato ya Mikoa hii haziwiani na hali halisi za maisha ya Wananchi wa Mikoa husika kwa fursa walizonazo. Mikoa niliyoitaja ndiyo inaongoza kwa eneo kubwa la Ardhi nzuri na idadi kubwa ya Mifugo Nchini ambayo pia ina fursa kubwa ya kuwaongezea Mapato. Pia Mikoa hii ina idadi kubwa ya Wananchi wanaojishughulisha na Kilimo cha Mazao yenye tija kubwa kama vile Pamba, Karanga, Alizeti na Ufuta. Aidha, biashara imeshamiri sana kwenye Mikoa hii, hivyo hakuna sababu ya Mikoa hii kuwa nyuma katika kipato cha Mwananchi. Vilevile, Mikoa mingine yote inayo fursa tele za kuwaongezea Wananchi wake Kipato na kupunguza Umaskini.


From: PM Mizengo Pinda speech of August 26, 2011


Takwimu hizi zaonesha ama kuashiria nini? kama hali ndo hii kwanini watu woote wasikimbilie Dar? maana ndo kwenye unafuu ati! wewe wasemaje? toa maoni yako tafadhari.  

No comments:

Post a Comment