Pages

August 2, 2011

UPUUUZI HUU WA WAZOA TAKA KIMARA B SALANGA UKOMESHWE!

Yapata miezi kadhaa sasa baadhi wakazi wa maoeneo ya Kimara B kata ya Salanga Jimbo la Ubungo wamekuwa wakiamka asubui na kukutana na marundo ya taka barabarani karibu kabisa na nyumba zao. 


Mwanzoni ilidhaniwa kwamba labda kuna gari la taka liliharibika na hivyo taka hizo kudondoka hapo, lakini kwa kitambo sasa imekuwa ni kama kawaida ni kama vile wazoa taka wa eneo hili wameamua kwa makusudi kubadilisha baadhi ya maeneo kuwa dampo, cha ajabu ni kuwa wanatupa taka hizo alfajiri kabla wakazi wa eneo husika kuamka ama kuwa wameshatoka. 

Baada ya kuchunguza kwa kitambo kidogo imegundulika kuwa wazoa taka hao wanafanya hivyo kwa makusudi katika zile nyumba ambazo hawapati ushuru wa taka kutokana na kuwa hakuna taka za kuzoa humo, nyumba hizi nyingi zina maeneo makubwa kiasi cha wenyewe kuchimba mashimo ya taka ndani ya fensi zao na wengine kutumia taka hizo kama mbolea, kitendo hiki ndicho kinapelekea wazoa taka wa Mtaa wa Salanga kuamua kwa makusudi kuchafua maeneo hayo kwa malengo binafsi kama picha hii inavyoonesha. 

Wakazi wa nyumba hii wameamka asubui na kukuta taka toka sehemu tofauti tofauti zimetupwa mbele ya geti lao, hii haiingii akilini, tunawaomba Viongozi husika wa maeneo haya kuanzia Mwenyekiti wa mtaa na diwani kupitia kwa Mbunge wa Jimbo John Mnyika kuongea na watu hawa na kukomesha vitendo hivi ambavyo si tu ni vya kipuuzi bali vya kishenzi pia. 

Wakazi wa Kimara B, Salanga. 

No comments:

Post a Comment