Pages

August 1, 2011

Tiba ya Babu wa Loliondo - Kuna shuhuda?

Tiba za VIKOMBEZ, JE kuna mtu mwenye ushuhuda?


Yapata miezi kadhaaa sasa toka kuibuka kwa taarifa za uwepo wa uponyaji wa magonjwa sugu, yaliyoshindikana hospitalini kupitia kikombe kimoja tu cha dawa ya mitishamba kikichanganjwa na maombi almaarufu “KIKOMBE CHA BABU” toka kwa Mch. Msaafu Ambekile Mwasapile huko Loliondo.

Mengi yalisikika mara baada ya kuibuka ama kuvumbuliwa KIKOMBE hicho, vyombo vya habari  vya ndani na baadhi vya nje vilielekeza macho, masikio na ama pua zake huko, na hivyo wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji wake kulishwa na kile kilichokuwa kikijiri huko, hii ilisababishwa umati wa watu toka pande zote za dunia kujaa kijijini Samunge kwa nia moja tu kupata kikombe.

Tulishuhudia mara ya baada Kikombe Cha Babu kuibuka na hatimaye kupata umaarufu mkubwa kupitia vyombo vya habari na zaidi kwa serikali karibu yoote kuelekea huko kupata kikombe, vilianza kuibuka vikombe vingine kila kona ya nchi yetu, woote wakidai kuwa “wameoteshwa” dawa ambayo yatolewa kupitia kikombe na kwa gharama kama ya Babu Tsh 500.

Imepita kitambo kidogo sasa hatujasikia kitu toka huko Loliondo ama kokote vilikoibuka vile “VIKOMBE”  vingine, ni takribani miezi mitano au sita toka tiba hizo au hiyo zianze kutolewa, tumesikia serikali na wataalamu wakitoa kila aina ya matamshi kuhusiana na tiba hiyo, nyingi zinajichangana ama kuwachanganya wanachi na zaidi wale waliowai kwenda kupata “kikombe” hiko.  

swali: Je hivi mpaka hivi sasa kuna mtu yeyote ana USHUHUDA wa nguvu kuhusu tiba hizi na zaidi ya Babu wa Loliondo?
Hii ni mbali na yule mama mmoja wa huko Samunge aliyedai kuponywa ukimwi.

Ikiwa kuna mtu anao ushuhuda, pliz tuwasiliane. 

No comments:

Post a Comment