Pages

February 22, 2011

Mkurugenzi Manispaa Zanzibar amwagiwa tindikali

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Rashid Ali Juma (45) alipomtembelea leo katika Hospitali ya Aga khan jijini Dar es salaam alikolazwa kwa matibabu kutokana na kuumia vibaya sehemu za usoni, tumboni, kifuani na ubavuni baada ya kumwagiwa Tindikali na Mtu asiyejulikana, wakati alipokuwa amekaa nje ya Msikiti wa Amani mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Insha saa 2:45 usuku, siku ya Alkhamis . Kwa muujibu wa madaktari wanaomhudumia Mkurugenzi huyo, wamemuambia Makamu wa Rais kuwa hali yake inaendelea Vizuri.

©VPO.

No comments:

Post a Comment