Pages

November 3, 2010

Zanzibar Mpya in the making

Chaguzi zipatazo tatu zilizopita huko Zanzibar kipindi kama hiki ilikuwa ni mshikemshike, hakukaliki, hakulaliki lakini sivyo ilivyo kwa uchaguzi wa mwaka huu, huko nyuma hukuwai kushuhudia wagombea kukaa pamoja kusubiri matokeo, zaidi kumpongeza aliyeshindwa, haikuwai kutokea, isipokuwa mwaka huu, kumbe tukiweka ubinafsi nyuma na kutanguliza utaifa haya yanawezekana.
Pongezi kwa Maalimu Seif kwa kukubali kiuungwana na pia Dr Shein kwa kuchaguliwa na pia kuwa tayari kufanya kazi na upinzani.
Sote twangoja kuona Zanzibar mpya yenye amani na utulivu zaidi yenye neema tele.

No comments:

Post a Comment