Pages

November 1, 2010

Chonde chonde NEC, Wagombea na vyama

Baada ya miezi zaidi ya miwili ya kampeni na hatimaye kuhitimishwa kwa Watanzania kupiga kura na hatimaye kuanza kuhesabiwa hapo jana kwa hali ya amani na utulivu kama ilivyodesturi yetu, jukumu pekee limebaki kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC katika kujumlishwa na kutoa na kutangaza matokeo rasmi na halali kwa kadiri yanavyopokelewa.
Pamoja na jukumu hili zito la NEC lakini jukumu kubwa pia liko kwa wagombea na vyama vyao pia, vyote kwa pamoja vinadhamana kubwa sana katika kuamua mustakbari wa taifa letu na kudumisha amani, katika ushindani wowote unaohusisha watu wawili au zaidi kuna kushinda na kushindwa, na wote wanaoingia katika ushindani wanatambua hilo.
Hivyo basi katika kipindi hiki ambapo tunasuburia kumalizika kwa zoezi zima la uchaguzi mkuu, kwa maana ya kutangazwa kwa matokeo rasmi, ni vyema viongozi, wagombea, vyama na wafuasi wao kuwa makini katika maamuzi yao mara baada ya kutangazwa matokeo rasmi, kwa uzoefu wa chaguzi nyingi hasa barani Afrika hiki ndicho kipindi kigumu kuliko vyoote vilivyopita, hapa ndipo uvumilivu na ukomavu wa kisiasa unatakiwa kuoneka.
Kushinda ni kuzuri na kushindwa si kuzuri, lakini yote ni matokeo tarajiwa katika ushindani wowote ule kama ilivyoelezwa mbeleni, ni vigumu sana kukubali kuwa umeshindwa pale ambapo unaamini kuwa umeshinda lakini mwisho wa siku ni lazima awepo mshindi, hivyo basi rai yangu kwa wagombea wooote kuonesha ukomavu wa kukubali matokeo yatakayotangazwa kwa moyo mnyoofu kabisa na kupeana mikono na mshindi, kwani hii ni siasa tu, ni uchaguzi wa mara moja kwa miaka mitano, ukishindwa sasa waweza jaribu tena.
Ni vyema pia wagombea wale watakaoshindwa wakasikiliza sauti za dhamiri zao ndani yao, wakatafakari mustakbari wa Taifa na maslahi yake badala ya maslahi binafsi kabla ya kusikiza ushauri wa wapambe, jamaa, ndugu na hata wake zao ambao wanaweza kuwashauri vinginevyo na kujikuta anapelekea taifa hili kusiko tarajiwa, mifano tunayo mingi tu na sehemu nyingi, jirani zetu ni mfano hai wa yale ambayo yalitokea katika kipindi kama hiki.
Pamoja na rai ya kuvitaka vyama na wagombea kukubali matokeo kwa moyo mmoja lakini ni vyema NEC ikaweka mazingira ya wagombea kukubali matokeo hayo kwa kuwa wawazi zaidi ili kutoa mwanya wa mtu kuhisia jambo, japo ni vigumu kuridhisha kila mmoja lakini kwa kuweka mambo wazi zaidi kunazuia uwezekano wa mtu kuwa na mashaka.
Tukumbuke kuwa uchaguzi, wagombea, vyama, tume, nk vitapita lakini Tanzania itaendelea kuwepo vizazi na vizazi, maamuzi yoyote katika woote hao maslahi na mustkbari wa TAIFA ndo ututangulie. chonde chonde NEC tupitisheni salama katika kipindi hiki tete.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Picha na lifetime blog

No comments:

Post a Comment