NEC imemaliza kazi muda si mrefu kwa kumtangaza Mgombea wa CCM Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais 2010 - 2015 kwa ushindi wa kishindo asilimia 61.17 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Dr Wilbrod Slaa.Tume iritarajia wapigakura Milion 20 lakini waliojitokeza ni asilimia 42% tu yaani Milion 8, wapigakura hawa hawafikii idadi ya waliopiga kura mwana 2005 kama takwimu zinavyoonesha hapo juu.Je nini kimetokea? kuna ugonjwa gani wa ghafla umewapata watanzania ata wasitokee kupiga kura? Je idadi hii ya watu waliojiandikisha ina walakini? NEC watakuwa na majibu na pengine maswali mengi zaidi ambayo yatazidi kuibuka kuhusiana na hili.Nampongeza Mh JK kwa kupata nafasi ya kuongoza tena ama kumalizia kipindi chako cha pili kwa mujibu wa katiba. Hongera sana na MUNGU akubariki katika utekelezaji majukumu yako.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment