Pages

November 6, 2010

Hizi ndoto nazo!!1

Usiku nimeota, ngoja hivi kuna ubaya kumuhadithia mtu ndoto yako? Kama upo mtanisamehe, maana hataYusufu wa biblia (Bwana Ndoto) asingehadithia nani angekumbuka baada ya ndotoze kuwa kweli?

Basi usiku nikaota tunazungumza mimi na mimi mwingine, yaani nafsi mbili ndani yangu zinabishana kuhusu yaliyotokea mchana wake, tukiwa tunapata Aloe Vera juice pale sebureni, sijui kama na wengine inawatokeaga hii ya mtu mmoja kujiona mko wawili au zaidi na kuanza kubishana ama kupingana katika jambo Fulani, sijui.

Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Mimi mwingini (MM): Duh kumbe kupiga kura huwa ni kwa zamu hapa bongo? Wale wazee wa SHINGO wana akili sana.

Mimi (M): Unamaanisha nini? (Maana ni kawaida yetu bongo kujibu swali kwa swali, si ndio?)

MM: Tena wale wazee waongezewe miaka mpaka ifike 50,

M: Mbona sikuelewi?

MM: Eeeh waongezewe ifike kama miaka ya Chama Cha John.

M: Mhh Chama Cha John? Ndo Chama gani? (Nikakumbuka mhariri wa gazeti moja pale lugoda.)

MM: Kwani wale SHINGO wamesema watu wangapi wa kupiga kura?

M: Si walisema ni Milion ishirini! Kwani vipi?

MM: na walioenda ni wangapi?

M: wamesema ni milioni nane, (huku najiuliza anaelekea wapi huyu)

MM: na mwaka uleee walipiga wangapi?

M: upi, wamaanisha 2005?

MM: Enhee huo huo,

M: Mhh sikumbuki vizuri sijui kumi na ngapi vile!

MM: ni karibia kumi na mbili milioni.

M: Aahaa, ok, sasa wasemaje? Maana naona wanzeveza tu, (Nikamswali kidogo maana naona ananipotezea)

MM: yaani we ujaona kitu hapo, ujaelewa bado? Ndo maana ulikuwa unapishana na mwalimu wa hesabu mlangoni weye.

Hapa ilibidi nihamaki kidogo kwani niliona sasa tunavunjiana heshima, maana wife nilimwambiaga mi ni mkali wa mahesabu na skuli nilikuwa naongoza na Junia anajua hivyo sasa huyu MM anataka kuniumbua, haiwezekani wacha nimkomeshe akalale.

M: we hebu koma kabisa mambo ya shule na haya unayonieleza yanauhusiano gani? Ka umelewa na hiyo AV juice si ukalale tu.

MM; akasogea karibu kabisa katika kochi nililokaa akanihonesha hesabu alokuwa anapiga.

MM: hebu angalia hapa, hii ni 20 ukitoa 8 si inabaki 12?

M: Ndiyoooo bwana sema unachomaanisha, (nikawa mkali kidogo, ati najikalikia mwenyewe)

MM: sasa hapa si inamaana waliopiga 2005 yaaani 12 hawajapiga mwaka huu, kwa hiyo watapiga tena kura 2015 na waliopiga mwaka hawatapiga 2015 mpaka 2020.

M: hapana we ujaelewa, hii ni idadi ya mwaka huu, ndo makadirio yake na sio ya mwaka 2005.

Ikabidi nijaribu kumfafanulia MM, akukubaliana nami, nikamweleza kuwa hakuna kitu kama zamu, bali kila mtu akifikisha umri wa kupiga kura anajiandikisha wakati ukifika anapiga kura, na kuwa mwaka 2015 watu watakuwa wengi zaidi ya hao, (Labda watakuwa au hatakuwa wengi maana nami sijui pia) kwa hiyo hao 12 hakutokea tu mwaka huu, wamekacha, labda wameogopa mabomu.

MM: Haiwezekani, mi nilienda saa kumi na moja na nikakuta watu washajaa, mabomu gani unayosema?

M: sisemi kuwa yalipigwa, bali najaribu kuwaza tu.

MM: mi nasema sio kweli, kwanza mwaka ndo watu wangekuwa wengi sana maana kila tulikokuwa tunapita wimbo ndo huo huo “JITOKOJENI” sasa iweje wasijitokeze?

M: we si wajua wabongo walivyo wagumu, (hapa nshachoka natamani kwenda kulala)

MM: au ile sunami ya kule visiwa vya mbali ilipiga wapiga kura wetu?

M: sio rahisi ni mbali sana kule.

MM: sasa ni kimetokea?

M: Sijui bwana,

MM: au ni wale wanafunzi waliolikizo? Au kina baba mmewazuia wake zenu kupiga kura kama kule mji wa mawe?

M: bwana we sikiza, mi nilienda na waifu sawa, afu wanafunzi hawafiki hata laki sembuse million.

…mara ghafla naamshwa na waifu, naulizwa

W: haniii! nikutengenezee supu ya pweza au? (Maana supu hii utengezwa siku ambayo sitoki home, sababu? Anajua mwenyewe)

M: Ndio, aaah hapana, vifaa vyangu viko wapi?

W: vifaa waenda wapi tena?

MM: Si kibaruani, hujui mwenye nyumba anakula kichapo aaah no kiap oleo?

W: we unaota Mwaka wa 2 huu ujaendaga huko leo iweje?

M: aah shit, nikakumbuka kumbe sikuizi siitaji kukurupuka tena alfajiri, naweza panga muda na siku ya kufanya kazi ama kupumzika na na bado naingiza mahela kama kawa, naweza amua cheza na waifu kutwa nzima na bado Rex Maughan anaingiza pesa kwa akaunti yangu na waifu na bizinesi yaendelea mtandaoni, masaa 24 siku 7 kwa mwaka!

Ningali nawaza ndoto ile ina maana gani?

Ndoto nyingine bwana!!!

Asante yesu.

No comments:

Post a Comment