Pages

June 16, 2010

Shibuda aingia mitini

MBUNGE wa Maswa, John Shibuda (CCM), a
metangaza kuondoa kusudio lake la kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Shibuda alitangaza nia yake ya kugombea kwa mara ya mwaka Oktoba mwaka jana na kurejea azma yake hiyo tena Mei 13, mwaka huu.
Lakini jana akitangaza uamuzi wake huo aliouita kuwa ameahirisha kugombea nafasi hiyo na atagombea tena mwaka 2015, alisema amefikia hivyo baada ya kuona Rais Jakaya Kikwete amefanya mambo mengi mazuri ya maendeleo.
“Napenda kutamka nina furaha kubwa ya kuongozwa na Rais Kikwete kwa sababu apendaye kuongoza lazima awe tayari kuongozwa na hisia za umma”, alisema
source: Habarileo

No comments:

Post a Comment