Pages

May 4, 2010

JK- TUCTA WAONGO, WANAFIKI, WANATUMIWA, WANA HIANA....

“TUCTA ni waongo! Tucta ni wanafiki! Tucta wana hiana!... wafanyakazi watakaogoma tarehe 5, watakuwa wamekiuka sheria na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni za Serikali. Na wale wafanyakazi wataokwenda kazini lakini wasifanye kazi, pia watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
“Kiongozi bora ni yule anayewaeleza wananchi wake ukweli hata kama ukweli huo utakuwa unauma.”
Hiyo ni kauli nzito ya Rais Jakaya Kikwete, alipozungumza na Taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam jana, kuhusu mgomo ulioitishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuanzia kesho, kwa madai kuwa Serikali imepuuza mapendekezo ya kuongezwa kwa kima cha chini ya mshahara kufikia Sh 315,000 kwa mwezi.
SOMA ZAIDI KAULI ZA JK vs TUCTA
TUCTA NI WAONGO - JK
JK - NIPO TAYARI KUKOSA KURA ZENU!
JK - MAY 5 STRIKE ILLEGAL
HAIJAPATA KUTOKEA
JK - STRIKE AND YOU'RE FIRED!
KIKWETE AZIKATAA KURA ZA TUCTA

No comments:

Post a Comment