Pages

August 19, 2009

Hili la CCM na UFISADI Limekaaje wadau?

HALMASHAURI Kuu ya CCM juzi ilifikia uamuzi wa aina yake baada ya kuunda kamati maalumu ya kuwashughulikia wabunge wake wanaoikosoa serikali ya chama hicho tawala, huku ikimwekea kinga rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
“Bunge limeanza kuwa kama mchezo wa (kikundi cha televisheni cha vichekesho) The Comedy,” alisema katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.
“Yaani kila mtu anafanya mambo yake mwenyewe, hali ambayo inaweza kusababisha watu kurushiana hata viatu ndani ya Ukumbi wa Bunge, sasa hali hii maana yake nini? “Kwa hiyo tumesema inatosha, hapo tulipofikia tusiendelee mbele.
Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo limejiona kama ni wateule wa kuzungumzia sakata hilo (la ufisadi) bila ya kujua wabunge wote wana haki ya kuzungumzia suala hilo, lakini kwa utaratibu tena kwa kupitia katika vikao vya kamati za wabunge.”
source: mwananchi

No comments:

Post a Comment