Pages

June 26, 2009

Tapeli huyu anastahili nishani!

Mama huyu aliyejitambulisha kwa majina kibao kama Judith, Rosemary, Mary nk. nadhani anastahili kupewa nishani ya ujasiri wa kitapeli kama ipo.
Mama huyu amekuwa akijitambulisha kama ni Afisa wa polisi wa cheo cha ASP, kikubwa zaidi ni ujasiri wake wa kwenda kujichanganya na polisi halisi na kuwatapeli mapesa kwa namna za udanganyifu tena Sentro Polisi, kafika mpaka kwa Kova mwenyewe kutaka kumtapeli lakini mzee mzima akastikuka.

2 comments:

  1. Kaka, heshima kwako. Ni muda sijakanyaga hapa barazani na nimeona mabadiliko. Naona hata taswira yako uko full na lens kali. Kwa sisi walevi wa taswira, hiyo inatamanisha saaana.
    Kuhusu huyu Mama nadhani kabla hajapewa nishani, ni lazima wengine waachie ngazi. Yaani mpaka anafikia hatua ya kwenda kwa Kova unadhani ameshapitia na kupokea taarifa ngapi za siri kuhusu polisi?
    Anyway. Blessings

    ReplyDelete