Pages

June 6, 2009

Nani anamajibu kwa Padri Karugendo??

NIMEAMUA kuuliza maswali haya, maana ni lazima atokee mtu wa kuyauliza. Haiwezekani tukasubiri miti na mawe kuuliza maswali haya. Kila Mtanzania aliyesoma, kila Mtanzania anayeguswa na uhai wa taifa letu, ni lazima ayaulize maswali haya.
Nauliza: Tumewaona mawaziri wa serikali ya awamu ya nne wakipiga kampeni kule Busanda. Walifanya hivyo kwa vile wao ni wanachama wa CCM au kwa vile wao ni watumishi wa umma? Kama walikwenda kama wanachama wa CCM, je walikuwa kwenye likizo? Tunaweza kuhakikishiwa bila mashaka yoyote kwamba walikuwa kwenye likizo?
Nauliza: Busanda walijiandikisha wapiga kura zaidi ya 100,000 lakini waliopiga kura ni 55,000 hawa wengine zaidi ya 50,000 wamepotelea wapi? Kwa nini hawakupiga kura? Hii ni idadi kubwa sana. Haiwezaekani kwamba hawakupiga kura kwa sababu ya ugonjwa- vinginevyo tungetangaziwa kwenye radio ugonjwa huo ulioikumba Busanda.

No comments:

Post a Comment