Pages

April 9, 2009

DECI - WHO'S IDEA IS THIS??

WACHUNGAJI na maaskofu zaidi ya 30, wa Kanisa la Pentekoste, wametoa tamko zito na kumtaka Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuingilia kati kuinusuru Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), ili iweze kuendelea na kazi yake ya kuondoa umasikini kwa Watanzania.
Maaskofu hao walitoa tamko hilo jana katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam, walipokuwa wakitoa msimamo wao kuhusu sakata hilo. Baadhi ya maaskofu hao ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati maalum waliyoiunda, Askofu Bartholomeu Sheggah, Katibu wa Kamati, Bernard Kung’unde na Askofu David Mwasota ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT)......ifate hapa
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa taasisi hiyo inayoundwa na Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walisema tasisi hiyo ilianzishwa baada ya kubaini kuwa vyombo vingi vya kuinua uchumi vilivyoanzishwa nchini vilikuwa vikijali faida kubwa kuliko kuwatetea wanyonge. Akisoma tamko la Deci kwa niaba ya wenzake, maaskofu hao, Bathromeu Sheggah, alisema inasikitisha na inakatisha tamaa kuona kwamba kwa kipindi cha miaka isiyopungua mitatu ya huduma ya taasisi hiyo, Benki Kuu (BoT) inatangaza katika vyombo vya habari kuwa taasisi yao haitambuliki. Alisema tangu waanzishe taasisi hiyo, Serikali imefanikiwa kupata zaidi ya Sh120, 674,497 milioni kama kodi ya mapato na kuwa wafanyakazi 400 wa taasisis hiyo wamekuwa wakilipiwa kodi ya mapato ‘PAYE’ na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Alisema ikiwa serikali italazimisha kusitisha kwa huduma za taasisi yao, wananchi wapatao 3,500,000 toka kwa washiriki wao 700,000 wataathirika kiuchumi, kiafya, kielimu na kijamii na hatimaye kuchangia vunjivu kwa amani ya nchi.
......Wakati viongozi hao wakizungumza na wadau hao, hakuna kiongozi wa DECI aliyehudhuria mkutano huo na baadaye Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Timoth ole Loiting’ye, aliiambia HabariLeo kwa simu kuwa hana taarifa ya mkutano huo, na kwamba maaskofu hao waliuandaa mkutano kwa utashi wao. “Sisi hatujawatuma wameamua wenyewe kuzungumzia suala hili, kwa sababu wamekuwa ni wateja wetu wa muda mrefu na tumewahudumia vizuri,” alisema na kuongeza kuwa DECI itatoa tamko lao.
..........HATIMAYE siri imefichuka kuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), inayojishughulisha na biashara ya kupanda na kuvuna pesa, ilianzishwa nchini mwaka 2007, baada ya kampuni yenye mfumo kama huo kufa huko nchini Kenya na kuwadhulumu maelfu ya wanaupatu wake waliokuwa wamejiunga nayo.
Vyanzo mbalimbali vya kuaminika, vimelitaarifu gazeti hili kuwa, raia mwema mmoja, jina tunalo, ndiye anayedaiwa kufichua siri ya DECI, kupitia barua pepe yake aliyoiandika kwenda kwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana nchini (CMSA), akieleza kuwa kampuni hiyo inaendesha biashara haramu kwa mfumo unaoitwa piramidi au upatu.

YOOOOOTE HAYA NNA SWALI MOJA TU.
JE DECI NI WAZO LA NANI HASA?
JE NI LA MAASKOFU AU KINA Mtaresi na Timoth Ole Loutingaye??
Baba Askofu Shegah na Mwasota je ni wazo lenu hili?

No comments:

Post a Comment