Usafiri wa wanafunzi ktk jiji hili umekuwa ni kasheshe kiasi cha watu wenye malori, japo yamepakia mzigo kulazimika kuwaonea huruma na kuwasaidia, lakini nadhani tutakubaliana kuwa hii si njia njema ya usafiri na pia ni hatarishi na je iwapo litatokea la kutokea (Mungu apishie mbali) tutamlaumu nani? tutamnyooshea nani kidole?
Hivi yale mabasi au mradi wa wanafunzi ulikufakufaje vile? maana hata screpa zake sizani kama zaweza kuonekana!
Je nini kifanyike kabla mambo hayajaharibika??
No comments:
Post a Comment