Rais Jakaya Kikwete akiagana na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda au"Mtoto wa Mkulima" na viongozi mbalimbalia katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda Comoro ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu.
Kuna haja ya rais kupokewa na uongozi wote wa nchi?
ReplyDeleteNi kitu ambacho sielewi kabisa,je kuna haja kweli ya Rais kila anapokwenda ziarani nje ya nchi na kila anaporudi kupokelewa na uongozi wote wa nchi?kwa sababu gani hasa?maana unaona kuna Waziri Mkuu,Mkuu wa Mjeshi,Mkuu wa Polisi na viongozi wengine kedekede.kwani hawa hawana kazi nyingine ya kufanya?mi nadhani Rais angeweza kabisa kupokelewa na mtu kama Mkuu wa Mkoa,nayo inatosha sana...
sijui wadau mnaonaje?!
Mdau Paesulta
(Kwa majadiliano zaidi tembelea jamii forum,kuna mjadala mrefu zaidi)