Hapa ni jijini Bongo, kijana katwumwa maji kwa matumizi ya nyumabani!! USALAMA? wauliza usalama? we watokea wapi? hapa ni bora liende tu.
Hili ndo Jiji la kwanza na la Biashara ambapo afisi zote muhimu ndipo zapatikana, pia ni makazi waheshimiwa wote wa nchi hii lakini maisha ndo ka hivyo, Je vijijini kukoje wadau? kama jijini maji yaweza kosekana kwa zaidi ya wiki tatu na bado twaona sawa au wahusika waona ok? je mikoani si ni kasheshe? Maji sasa yauzwa ndoo 1 shs 500 hadi 2,000!!!!! ndoo ya lita 20 tu je wangapi waweza kumudu maisha hayo? WADAU MNA MAONI GANI?
No comments:
Post a Comment