Pages

November 12, 2008

Nyaulawa aagwa Dar

RAIS Jakaya Kikwete pamoja na mkewe Mama Salma leo wameongoza mamia ya waombolezaji wakiwamo viongozi wa serikali, wabunge na wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa (57) aliyefariki dunia Jumapili nyumbani kwake, Kawe Beach, Dar es Salaam. Mwili wa marehemu Nyaulawa umeagwa kwa Ibada ya Misa iliyoongozwa na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha, Mikocheni, Padri Paul Haule na kisha heshima hizo za mwisho.

No comments:

Post a Comment