BAADA ya wanafunzi kugoma kuingia madarasani Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani umewasimamisha masomo wanafunzi wote wa shahada ya kwanza kwa mudu usiojulikana. Hatua hiyo imechuliwa baada ya wanafunzi hao kukaidi agizo la Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe la kuwataka warejee madarasani jana ifikapo saa moja asubuhi. Hata hivyo wanafunzi hao waliendelea na mgomo huo hali iliyolazimu uongozi wa chuo hicho kuchukua hatua za kuwasimamisha kwa lengo la kurejesha amani chuoni hapo. Wanafunzi hao wapatao 16,000 waliamuriwa kuondoka maeneo ya mlimani ifikapo saa 12 jioni. Polisi walitumika kuhakikisha wanafunzi hao wanaondoka maeneo hayo bila kufanya uharibifu wowote. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya wanafunzi hao kukiuka sheria za chuo hicho kwa kutoingia darasani kwa siku tatu mfululizo kwa madai ya kupinga sera ya uchangiaji na kutaka Serikali iwapatie mkopo kwa asilimia 100.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment