Pages

July 1, 2008

Bank Holiday??????????????????

Wadau naomba ufafanuzi au mnitoe ushamba kidogo, hii bank holiday ni nini hasa na inaunuhimu gani kwa taifa letu na ukuaji wa uchumi?
Leo hii mabenki yote yamefungwa sababu ya kitu inaitwa BANK HOLIDAY na ambayo sikumbuki kuisikia hapa bongo (kama kumbukumbu zangu zi sahihi) na leo BOT imewaamrisha wateja wake woteeee kufunga shughuri zao
Swali: watanzania wengi bado twatumia sana cashi kufanya manunuzi yetu ya kila siku tofauti na mataifa yaliyoendelea, Je hii haimaanishi kuwa wafanyabiashara kadhaa leo hawatalala kwa amani kwa kuofia kuja kuporwa mauzo yao ya siku?
Na je hiki si kichocheo cha ujambazi?
Naomba kuelimishwa wadau.Posted by Picasa

No comments:

Post a Comment